Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Kaabi, mjumbe wa Uongozi wa Baraza la Wanazuoni, katika mkutano wake wa leo na kundi la walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Pasdaran), alisema: “Bibi Fatima Zahraa (a.s.) alikuwa mwenye kufanana zaidi na baba yake. Katika uongozi wa kimantiki na hoja pia alikuwa hivyo, na Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) alikuwa akimpa heshima ya kipekee.”
Akiashiria kwamba Bibi Zahraa (a.s.) alibeba dhima ya umma mzima wa Kiislamu, aliongeza: “Alikuwa ni mwanamke mmoja, lakini mwenye ustahimilivu mkubwa ambao mhimili wake ulikuwa ni utii kwa uongozi wa Kiwilaya.”
Ayatollah Kaabi aliendelea kusema: “Ustahimilivu wa Bibi Zahraa (a.s.) ulikuwa na baraka; miongoni mwa baraka zake ni Ashura, na miongoni mwa baraka zake pia ni kwamba ulimwengu utajaa uadilifu na usawa kwa kudhihiri kwa Mkombozi wa ulimwengu. Mapinduzi ya Kiislamu pia ni mwanga uliotokana na nuru ya ustahimilivu wa Bibi Zahraa (a.s.). Sisi tunahitaji subira ya Fatima na basira ya Fatima. (Fatimah alikuwa ni Siddiqah, shahiidah.)
Maoni yako